
Baba Mtakatifu Francis ametaka
viongozi duniani wanaoshiriki mkutano wa G20 mjini Brisbane kuwafikiria
watu masikini ulimwenguni.
Amewataka Viongozi hao kupata ufumbuzi wa kuimarisha hali ya maisha ya watu walio masikini.Viongozi wa nchi 20 zilizo na uchumi mkubwa wanakutana Brisbane nchini Australia mwishoni mwa juma hili kujadili maswala mbalimbali yahusuyo uchumi.
Kiongozi huyo wa juu wa kanisa katoliki amesema pia mkutano huo unatarajiwa kujadili hali ya mambo mashariki ya kati.
Amewataka viongozi kutotupia kisogo maisha ya watu yaliyo hatarini na kuonesha matumaini kuwa mkutano huo utatathimini kuinua maisha ya watu walio masikini na kupiga vita hali ya ukandamizaji ambao haukubaliki.
Mkutano wa G20 utaanza siku ya jumamosi.