Baada ya safari ya miaka kumi katika
anga za juu, chombo cha anga za mbali cha Ulaya kimevuka kilomita
chache za mwisho kutoka ardhini kutekeleza kile kitakachokuwa kifaa cha
kwanza kuwahi kutengenezwa na binadamu kutua kwenye kimondo.
Roboti
hiyo iliyotengezwa Ulaya kwa jina Philae, imefanikiwa kutua katika
kimondo likiwa ni jambo la kihistoria kuwahi kushuhudiwa. Aidha roboti hiyo ilitua katika Kimondo kinachojulikana kama 67P/Churyumov-Gerasimenko saa kumi jioni saa za Ulaya.