Mazishi ya kitaifa yanafanyika
nchini Zambia kumuaga hayati Rais wa nchi hiyo Michael Sata aliyefariki
hospitalini mjini London Uingereza mwezi jana.
Sata alikuwa na umri wa miaka 77.Katika wiki chache zilizopita, wanachi wamekuwa wakitoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo ambaye mwili wake ulikuwa umelazwa katika majengo ya bunge.
Rais Sata alifariki akipokea matibu
Mazishi yanayofanyika mjini Lusaka yatahudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kikanda.
Rais Sata atazikwa katika eneo lenye makaburi yaliyotengewa Marais wa nchi hiyo.
Taifa hilo kwa sasa linaongozwa na kaimu Rais huku uchaguzi mkuu ukipangwa kufanyika katika muda wa miezi michache ijayo.