
Kocha wa England Roy Hodgson
amemsifu nahodha wa timu hiyo ya taifa Wayne Rooney kabla hajacheza
mechi ya 100 katika michuano ya michuano ya ulaya mwaka 2016, ambapo
England itakutana na Slovenia.
Rooney (29), alianza kuichezea timu ya England akiwa na miaka 17 mwaka 2003 na ni mfungaji wa nafasi ya nne akiwa ashatia nyavuni magoli 43.
Rooney ana kadi sita nyekundu, mbili akiwa na England, Hodgson ameeleza. Kazi yake hii imekuwa na vikwazo ya kila namna lakini imemkomaza na kumkuza kiakili.
Akizungumza na Radio 5 ya BBC, Hodgson amesema kuwa Rooney ni mkombozi wa soka la uingereza, huhakikisha kuwa kila mmoja yuko sawa na anaridhika na kuhakikisha kuwa hakuna tatizo ndani ya kikosi.