Wanaharakati watatu wa kisiasa
nchini Libya wamechinjwa baada ya kuandika katika mitandao ya kijamii
juu ya maisha chini ya utawala wa dola ya kiislam.Miili yao ilipatikana
mapema wiki hii mashariki mwa mji wa Derna karibu na Benghazi.
Tukio
hilo lilianzia kwa wanaharakati hao kutekwa mapema mwezi huu.Mji huo wa
Derna uko chini ya mamlaka ya kikundi cha dola ya kiislam tangu mwaka
2012 ambacho kimekiri kuwa sehemu ya kundi la is.Mnamo mwezi August mwaka huu katika video ilooneshwa katika mitandao ya kijamii ilionesha mwanamume mmoja akipigwa risasi na kufa hadharani katika viwanja vya mpira mjini Derna.
Siku za hivi karibuni kuna picha iloachiliwa mitandaoni ikionesha kikundi cha kijamii kinachojiita mahakama ya kiislam.